JESSICA COX, RUBANI MWANAMKE ASIYE NA MIKONO


Rubani huyu alizaliwa bila mikono kutokana na ‘Genetic defects’, haruhusu hali hiyo kumzuia kuishi maisha ya kukata tamaa. Yeye ndiye wa kwanza mwenye leseni ya urubani japo bila mikono.
Ana mkanda mweusi katika taekwondo na hufanya shughuli zingine kama mtu mwenye mikono yote. Hupiga piano na vile vile kupiga mbizi. Jessica ni ‘MOTIVATIONAL SPEAKER’ anayeishi kwa mifano hai. Alisema watu wengi huwa wanamuona akiwa hana mikono kama sababu ya kuzuia, lakini yuko hapa ili kuwathibitishia wote kuwa hawakosei.
Alipata leseni yake mnamo Oktoba 10, 2008 baada ya kupata mafunzo kwa miaka mitatu. Roho yake ya uthubutu siku zote imekuwa dhahiri kwake. Na mnamo mwaka 2015 aliandika kitabu, Disarm your limits, kitabu kinachoelezea maisha yake. Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Arizona mnamo 2005 na digrii katika saikolojia na mdogo katika mawasiliano.

No comments

Powered by Blogger.