TANZANIA INAHITAJI 'LIL OMMY' NA 'SALAMA JABIR' WENGI ZAIDI

"Mafanikio huja kwa kufanya unachokipenda", hii ni kwa mujibu wa Fid Q na wanafalsafa wengine wengi ambao wamepata kiutokea katika uso wa dunia. Tasnia ya habari (hasa habari za burudani) kuna sehemu inapwaya. Hii ni kutokana na watangazaji wengi kufanya kazi zao huku kipaumbele kikubwa ikiwa ni pesa. Nafahamu kila mtu anapenda pesa kwa namna moja au nyingine lakini kuna mahali inafika pesa si kitu kwani unaweza kuwa na pesa zote za dunia lakini bado kuna vitu ambavyo pesa haiwezi kununua ukawa huna (uhai, upendo, mapenzi ya kweli, n.k)..
Pale nnaposema tasnia ya habari (burudani) inapwaya namaanisha kuna type ya watangazaji ambao wapo wachache ilhali wanahitajika wengi zaidi kama wao. Watu kama Lil Ommy na Salama Jabir ni aina ya watangazaji ambao Tasnia ya habari za burudani inawahitaji zaidi, kwani mtu kama Salama Jabir kipindi anafanya kazi EATV alikuwa mmoja kati ya watu waliokuwa wakikosoa sana video za wasanii wa Bongo hadi kufikia baadhi ya wasanii kutaka kumpiga (ukweli unauma). Hii imechangia kwa kiasi kikubwa wasanii kufanya video nzuri na zenye ubora ambazo zinapigwa channels kubwa duniani. Kwa upande wa Lil Ommy ukisikiliza vile anauliza maswali utafahamu kama jamaa yupo smart upstairs na pia anaipenda na kufurahia kazi yake.
Lil Ommy instead of kuuliza "Wimbo wako wa kwanza unaitwaje" atakuuliza "Kwenye wimbo wako wa kwanza unaoitwa XXX ambao umeufanya kwa producer XXX umeongelea sana pesa, Je pesa ni kila kitu kwenye maisha yako". Hii ina maana mtangazaji amefanya reserch kuhusu muziki wako, ameandaa maswali na yupo tayari kwa ajili ya kukufanyia interview. Wengine kitakachokuja kichwani ndo kitu atauliza, this is wack. Salama kesha waponda sana kina Jay Moe (japokuwa alikuwa crush wake), Pasha, Ferooz, n.k kwa kuvaa hovyo kwenye video kitu ambacho ni nadra sana kuona kwa sasa. Kwa hayo machache bila shaka umuhimu wa watu kama Lil Ommy na Salama Jabir unaonekana kwenye tasnia ya habari za burudani na tunawahitaji wengi zaidi ili kukuza muziki wetu ukafika mbali zaidi. Adam Mchomvu (Clouds FM), Dullah (EA Radio), Yule jamaa wa Block 89 (Wasafi Radio) wanajitahidi sana lakini bado, nguvu zaidi inahitajika.

Next stopKupitia watangazaji makini, Dj's & Producers wakishirikiana na wasanii / wanamuziki tunaweza kupata identity ya muziki wetu. Wasikilizaji tumechoka kusikia wasanii / wanamuziki wetu wakiimba kama wa'south, wa'nigeria na wa'congo. We need our own sh*t #BongoFlava..!

No comments

Powered by Blogger.