HATIMAYE AKONSHAZ MUSIC WABADILISHA RASMI JIJI LA 'DODOMA'

Hatimaye wasanii kutoka Akonshaz Music wamefanikiwa rasmi kubadilisha jina la 'Dodoma' kimuziki na kutoa jina rasmi kwa jiji hilo. Kuanzia sasa Dodoma itafahamika kama 'Land of Albert - LA' ikiwa ni kutoa heshima kwa msanii Albert Mangwea ambaye anafahamika kama msanii pekee ambaye ametambulisha jiji la Dodoma kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya, kwa kulitambua hilo Akonshaz Music wameamua kutoa mixtape album ambayo inaitwa 'Land Of Albert - LA' ikiwa ni kutoa heshima kwa Albert Mangwea na pia kwa mashabiki wake ambao wanapenda muziki wa kizazi kipya. 
Mixtape album ya Akonshaz Music imetayarishwa na wasanii kama John MP, Creyz Biyz, Crown Jay, The Green na Cascos huku watayarishaji (producers) wakiwa ni Wi2 Touchez na Magnificent. Album ina nyimbo tisa (9) na nyongeza ya wimbo mmoja wa Mangwea ambao haujawahi kuusikiliza. 
Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.