NYIMBO 8 ZA KENDRICK LAMAR ZAVUJA MTANDAONI, IPO KOLABO YAKE NA MICHAEL JACKSON

Mwaka 2018 unazidi kuwa mwaka mzuri zaidi kwa wapenzi wa hiphop duniani kote baada ya wasanii wengi wa hiphop kutoa album akiwemo Eminem - Kamikaze, Lil Wayne - Tha Carter V, Drake na wengineo wengi ambao wanataraji kutoa album akiwemo Kanye West na T.I ambao album zao zipo mbioni kutoka kabla ya mwaka 2018 kuisha. 

Habari nzuri kwa wapenzi wa hiphop ambayo ni habari mbaya kwa msanii Kendrick Lamar ni baada ya nyimbo zake 8 kuvuja mtandaoni ikiwemo kolabo yake na Michael Jackson inayokwenda kwa jina la 'Look Over Your Shoulders'. Extended Play (EP) hiyo imepewa jina la 'Bad Kid Chill City'. Kama bado hujapata wasaa wa kuisikiliza weka comment yako hapo chini nikutumie link..
Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.