MATATIZO YA KIMTANDAO YASABABISHA ALBUM YA DODOMA - BEACH DUME KUCHELEWA KUTOKA, KUACHIWA RASMI IJUMAA TAREHE 29/04

Wakati mashabiki wakiendelea kuuliza kulikoni album ya Dodoma - Beach Dume ambayo ilitarajiwa kutoka tarehe 22 / 04 kushindwa kufanya hivyo, uongozi wa kampuni ya Alvial Tz ambayo mwaka huu imeshirikiana na BlackMutu kuandaa na kuachia album hiyo kwa awamu ya pili umejitokeza na kusema kuwa matatizo ya kimtandao ndiyo sababu pekee iliyosababisha kuchelewa kwa album hiyo ambayo itapatikana mtandaoni pekee. Kama hukupata nafasi ya kuisikiliza Domtown Stand Up album vol. 1 hii hapa kwa danta..
 BlackMutu aliongeza kwa kusema kuwa album hiyo ipo tayari na inategemea kuachiwa rasmi tarehe 29 / 04 saa 8 mchana kwa saa za Afrika mashariki. Pia aliwataja baadhi ya wasanii ambao nyimbo zao zitakuwepo kwenye album hiyo kuwa ni DDC (Dom Down Click), Gifted-son Coinboy, Bad Mc'z, KzK Musicians, Sharray, Creyz Beez, The Wiseman Gangstar, Vitamu Crew na Doxy wa Nigeria ambaye amefanya Kirikuu remix ya Moni wa Central Zone.

No comments

Powered by Blogger.